Tuesday, June 5

Kitunguu Swaumu hutibu magonjwa 30

Mungu anaposema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hamaanishi maarifa ya kutengeneza au kuendesha ndege, ni maarifa ya kawaida tu katika maisha yetu ya kila siku ambayo yanaweza kubadilisha afya na ustawi wetu.
Moja ya mmea ambao umependelewa sana na Mungu kwakuwa na viinilishe vingi na mhimu sana kwa afya ya binadamu ni kitunguu swaumu. Kitunguu swaumu ni dawa karibu kwa kila ugonjwa.
Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.
Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen’genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.
Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika nchini China mwaka 510 kabla ya Kristo na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Warumi.
Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana. Kuna baadhi ya imani watu wanaamini kitunguu swaumu kina uwezo wa kufukuza hadi wachawi! hivyo kama unatokewa unapata usingizi wa usioeleweka au unakabwa kabwa na wachawi hebu jaribu kitunguu swaumu na utuletee mrejesho
Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia.
Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash).
Huko sokoni tayari nimeviona vitunguu swaumu kutoka China na Afrika kusini ambavyo vyenyewe huwa vina punje kubwa nene na huwa rahisi kuvimenya, hata hivyo ili upate faida hizi zote hapa chini naendelea kukushauri utumie vitunguu swaumu vyetu vinavyolimwa hapa Tanzania kwani hivyo vya kutoka nje pamoja na kuwa ni rahisi kuvimenya lakini ubora wake si kama ule wa vitunguu vyetu.
Hakikisha kila mboga unayopika haikosi kitunguu swaumu ndani yake na ikibidi ukiweke mwishoni mwishoni unapokaribia kuipuwa mboga yako toka katika moto kwamba kisiive sana hata kupoteza viinilishe vyake.
Kama una friza au friji ya kawaida unaweza kumenya vitunguu swaumu hata kilo nzima na kuvitwanga kidogo katika kinu, vifunge vizuri katika bakuli au mfuko wa plastiki na uvihifadhi katika friza au friji na hivyo kila unapopika unachukuwa tu na kukitumia ili kuepuka usumbufu wa kukimenya kila siku.
Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji au ukichanganye na mtindi kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.
Namna ya kutumia kitunguu swaumu:
1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume haraka
2. Kigawanyishe katika punje punje
3. Chukua punje 6
Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume haraka
4. Menya punje moja baada ya nyingine
Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume haraka
5. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume haraka
6. Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala.
Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.
Fanya hivi kila baada ya siku 1 unapoenda kulala kwa wiki 3 mpaka 4. Unaweza pia kuendelea kukitumia hata kama unmepona tatizo lako.
Ukiona kichwa kizito au kinauma pumzika kutumia kitunguu swaumu kwa siku 3 hivi kisha endelea tena, mhimu usitumie kila siku bali ni kila baada ya siku 1.
Katika zoezi hili nimetumia mtindi wa Tanga freshi na nimeona matokeo mazuri sana ikiwemo ngozi kuendelea kung’aa na kitambi ni kama kimeisha kabisa kwa siku 7, hivyo siyo lazima uwe mtindi uliotengeneza nyumbani bali hata huo wa dukani wa Tanga fresh bado ni mzuri pia (bila shaka Tanga fresh watanipa hela ya soda kwa kuwapigia promo)!
Fanya hivi kila siku au kila mara unapopata nafasi na hivyo utakuwa mbali na kuuguwauguwa. Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema asitumie, kwa ujumla tu mjamzito uwe makini utakapotumia kitunguu swaumu kwa namna hii kama wewe ni mjamzito.
Lakini pia unaweza kupata kitunguu swaumu katika mfumo wa vidonge na ikawa rahisi kwako kutumia

Vidonge vya Kitunguu Swaumu
Kitunguu swaumu kinatibu magonjwa 30 yafuatayo:
mbegu-za-maboga
Magonjwa yaliyothibitika kutibika na kukingika na kitunguu swaumu ndani ya mwili:
  1. Huondoa sumu mwilini. Soma hii pia > Njia 16 za kuondoa sumu mbalimbali mwilini
  2. Husafisha tumbo
  3. Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)
  4. Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I. 
  5. Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine
  6. Huzuia kuhara damu (Dysentery)
  7. Huondoa Gesi tumboni
  8. Hutibu msokoto wa tumbo
  9. Hutibu Typhoid
  10. Hutibu mafua na malaria
  11. Hutibu kifua kikuu (ukitumia kitunguu swaumu kesho yake unaweza kutokwa na makohozi mengi tu ambayo ni ishara kwamba kweli kinatibu kifua kikuu (TB)
  12. Hutibu kipindupindu
  13. Huongeza SANA nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume). Soma hii pia > Tatizo la Nguvu za Kiume na Suluhisho lake
  14. Hutibu maumivu ya kichwa. 
  15. Hutibu kizunguzungu
  16. Hutibu shinikizo la juu la damu. 
  17. Huzuia saratani/kansa. 
  18. Hutibu maumivu ya jongo/gout. 
  19. Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
  20. Huongeza hamu ya kula
  21. Huzuia damu kuganda
  22. Husaidia kutibu kisukari. 
  23. Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi (ni kweli, na ni moja ya kazi nyingine ya kitunguu swaumu iliyonishangaza zaidi) pia kinaondoa msongo wa mawazo/stress na kukufanya uishi miaka mingi
  24. Huongeza SANA kinga ya mwili na kwa muda mfupi, kijaribu na ulete majibu. Soma pia hii >Vyakula 16 vinavyoongeza Kinga ya mwili
  25. Huvunjavunja mawe katika figo
  26. Huupa nguvu ubongo. Kazi nzuri niliyopenda zaidi katika kitunguu swaumu.
  27. Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu
Magonjwa yaliyothibitika kutibika na kukingika na kitunguu swaumu katika Ngozi:
28. Hutibu upele
29. Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi
30. Hutibu mba kichwani
31. Huondoa chunusi
32. Miwasho katika ngozi na sehemu za siri
33. Fangasi katika ngozi
34. Bawasiri ya nje
35. Pumu ya ngozi
36. Mikunjo na alama za kuzeeka mapema katika ngozi
37. Na maambukizi mbalimbali katika ngozi
Kwa mjibu wa utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha afya cha Maryland nchini Marekani (University of Maryland Medical Center), Kitunguu swaumu kina viinilishe ambavyo hudhibiti bakteria (anti-bacterial), fangasi (anti-fungal ), virusi (anti-viral) na vijidudu nyemelezi (anti-parasitic) sifa inazokifanya kiwe na uwezo wa kutibu ugonjwa wa matatizo mbalimbali katika ngozi.
Kitunguu swaumu kinao uwezo wa kuzuia usipate upele, mba, chunusi, mabaka mabaka na maambukizi mbalimbali katika ngozi na kukuacha na ngozi yako ya thamani ya asili na yenye kupendeza.
Ili kujitibu matatizo mbalimbali ya ngozi tumia kitunguu swaumu kwenye kila chakula unachopika, kitumie kibichi katika maji au mtindi na pia pakaa mafuta ya kitunguu swaumu kila siku katika ngozi yako na hutachelewa kuniletea ushuhuda hapa.
Kitunguu swaumu hutibu upele
Mafuta ya Kitunguu swaumu
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;
  • Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
  • Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
  • Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
  • Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila.
Nini madhara ya vitunguu swaumu?
Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;
  • Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa, kunywa maji mengi au kutafuna karafuu. Na nimeshuhudia nikinywa kwenye mtindi hii harufu ni kama haipo kabisa na hata ukijamba haikutokei ile harufu mbaya sana kama ukinywa vitunguu swaumu katika maji
  • Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
  • Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha. Ikikutokea kuharisha siku mbili tatu furahi kwani ni njia mojawapo ya mwili kujisafisha
  • Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
  • Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
  • Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
Kumbuka kitunguu swaumu kinaweza kuwa na faida nyingi zaidi ya hizi lakini bado nakushauri utumie kiasi kidogo (punje 6 tu) kila baada ya siku 1 kwa kipindi kirefu wiki 2 au 3 hata mwezi ili uone faida zake zaidi.
Ikikutokea tangu umeanza kutumia kitunguu swaumu kichwa kinauma zaidi unaweza kupumzika siku mbili hivi na baadaye unaendelea hivyo hivyo.

0 comments:

Post a Comment

Popular

Blogger templates

Blogroll

About

Buscar

Search This Blog

Blog Archive

Featured Post

Uhusiano wa vidonda vya tumbo na saratani ya tumbo